
Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) kwa mara nyingine tena jana Alhamisi lilithibitisha kuhusu mamlaka ya kujitawala na umoja wa arfdhi nzima ya Somalia na kutupilia mbali suala la kutambuliwa rasmi eneo la Somaliland kama nchi huru.
AU pia imelaani hatua za pande za nje za kuingilia masuala ya ndani ya Sudan kufuatia mzozo unaendelea nchini humo. huku kukiwa na mzozo unaoendelea.
Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limetoa taarifa ambapo kwa mara nyingine tena limekaani vikali na kupinga hatua ya upande mmoja ya Israel ya kuitambua rasmi kile kinachojulikana kama Jamhuri ya Somaliland na kutaka kufutwa uamuzi huo mara moja.
Baraza la Amani na Usalama la AU lilitamka jana katika mkutano wa ngazi ya mawaziri huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia kwamba hakuna pande yopyote iliyo na mamlaka au hadhi ya kubadilisha mpangilio wa kijiografia eneo la Nchi Mwanachama wa Umoja wa Afrika,” na kwamba tamko lolote kama hilo ni batili na halina athari za kisheria kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Baraza hilo aidha limeunga mkono na kukaribisha kufanikiwa hivi karibuni oparesheni za kijeshi za Somalia dhidi ya kundi la kigaidi la al Shabaab na kuwahimiza askari usalama wa Somalia wanaoungwa mkono na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika (AUSSOM) na washirika wengine kuendeleza oparesheni hizo ili kulitokomeza kabisa kundi la al Shabaab na makundi mengine ya kigaidi.