Kurugenzi Kuu ya Masuala ya Uchaguzi (DGAE) nchini Congo-Brazzaville imefunga kipindi cha usajili kwa wagombea kushiriki katika uchaguzi wa urais mnamo Machi 15. Angalau watu saba, akiwemo Denis Sassou-Nguesso, 82, rais aliye madarakani ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40, wamewasilisha maombi yao. Mbali na mkuu wa nchi, wagombea sita wa upinzani wanawania urais.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Denis Sassou-Nguesso ambaye alichaguliwa mwaka wa 2002 na kuchaguliwa tena mwaka wa 2009, aliweza kugombea tena na kushinda uchaguzi wa rais mwaka wa 2016 na 2021, kufuatia marekebisho ya katiba mwaka wa 2015 ambayo yaliondoa kikomo cha umri (miaka 70) na kuongeza hadi miaka mitatu idadi inayowezekana kwa muhula wa miaka mitano. Mkuu wa nchi anagombea tena.

Destin Gavet wa chama cha Movement of Republicans (MR) ni miongoni mwa wagombea wa urais nchini Congo-Brazzaville. Akiwa na umri wa miaka 35, bila shaka ndiye mgombea mweye umri mdogo zaidi na anagombea kwa mara ya kwanza, anaripoti mwandishi wetu huko Brazzaville, Loïcia Martial.

Pia miongoni mwa wagombea wanaogombea kwa mara yao ya kwanza ni Vivien Manangou, profesa wa sheria katika chuo kikuu cha umma, na Zinga Mabio Mavoungou, mbunge wa zamani. Hatimaye, pia kuna Dave Mafoula, ambaye tayari alikuwa mgombea mwaka wa 2021, Joseph Kignoumbi Kia Mboungou, ambaye alishidana na Denis Sassou-Nguesso katika kila uchaguzi tangu mwaka 2002, na Anguios Nganguia Engambé, mgombea kwa mara ya nne mfululizo.

Wagombea bado wanahitaji kuthibitishwa.

Wagombea hao lazima wathibitishwe na Mahakama ya Katiba kabla ya kuanza kwa kampeni mnamo Februari 28. Chama cha UPADS na chama cha UDH-Yuki, vyama viwili vikuu vya upinzani, havijawasilisha wagombea wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *