NAIROBI – Bunge la Umoja wa Ulaya linataka uchunguzi huru na wa haraka  kufanyika dhidi ya kile limetaja kuwa uhalifu wa kibinadamu unaotekelezwa na idara ya usalama na viongozi wa kisiasa nchini Uganda.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika kikao cha Alhamisi, bunge hilo limetia wasiwasi ushindi wa rais Yoweri Museveni, na kusema uchaguzi wa mwezi uliopita uligubikwa na ukiukaji wa haki za kibinadamu, vitisho, wizi wa kura, vurugu na kufungwa kwa mitandao.

Bunge hilo pia linataka viongozi wa upinzani ambao bado wanazuiliwa kuachiliwa huru na vitisho dhidi ya kiongozi wa upinzani Bobi Wine na hulka ya matumizi ya vurugu wakati wa uchaguzi kukomeshwa mara moja. Wabunge 514 wakipiga kura kuunga mkono hoja hiyo huku 56 wakikosa kushiriki.

Aidha, bunge hilo pia limeeleza wasiwasi kuhusu kufungiwa kwa mashirika ya kiraia na matumizi ya mahakama ya kijeshi kusikiliza kesi dhidi ya raia na pia kutoa taarifa zote kuhusu raia waliopotea.

Kauli ya Bunge la Ulaya inajiri kipindi hiki kiongozi wa upinzani Bobi Wine akiwa bado yuko mafichoni baada ya uchaguzi wa mwezi uliopita akihofia kukamatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *