#HABARI: Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Tandaimba mkoani Mtwara limepitisha bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 46 kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha.

Katika bajeti hiyo, zaidi ya shilingi bilioni moja imetengwa mahususi kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa soko la Forodhani ambalo linatarajiwa kuwasaidia wajasiriamali wadogo kuboresha mazingira yao ya biashara.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, David Sianya, amebainisha kuwa bajeti hiyo imezingatia vipaumbele vyote vilivyomo kwenye mwongozo wa Serikali, huku baadhi ya vijana wakieleza kufurahishwa na kasi ya miradi inayotekelezwa kwa mapato ya ndani.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Juma Mmange, amesisitiza umuhimu wa kusimamia vyema utekelezaji wa mipango hiyo ili kuleta tija ya kweli kwa wananchi wa Tandaimba.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *