#HABARI: Jopo la Mawakili wa Makamu Mwenyekiti Mstaafu Wa Chadema- Zanzibar, Said Issa Mohamed na Wenzake ambao ni Mawakili Waandamizi Shabaan Marijani, Gido Semfukwe Na Alvan Fidelis Wamesema Chama cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA) Bado hakitakiwi kujihusisha na masuala ya siasa na kutumia mali za Chama kwa sababu Amri ya Mahakama ni kwamba ukomo wake ni hadi pale kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Wakili Semfukwe alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na tamko lililotolewa Januari 23,2026 na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Dk Rugemeleza Nshala, kwamba zuio la kufanya shughuli za kisiasa kwa Chadema lilikoma Disemba 10,2025 ikidaiwa ni miezi sita tangu zuio hilo lilipowekwa na Mahakama Kuu.
Aidha, imeelezwa kuwa zuio lilitolewa chini ya Kifungu 1 (a) na 1 (b) ya Sheria ya Mwenendo wa Madai Sura 33 inayobainisha kuwa zuio linalotolewa chini ya kanuni hiyo linadumu hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania