#HABARI: Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Mhe. Geofrey Mdama, amefungua kikao kazi kati ya TANESCO na viongozi wa Serikali za Mitaa, Kata, na Madiwani mkoani humo.
Katika hafla hiyo iliyofanyika Februari 12, 2026, Meya Mdama amepongeza mchango mkubwa wa nishati ya umeme katika kuchochea ukuaji wa uchumi, viwanda, na uwekezaji kwa wananchi wa Singida.
Mhe. Mdama amekipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa uamuzi wa kuwashirikisha viongozi hao wa ngazi za chini, ambao ndio kiunganishi kikuu cha kutoa elimu kwa jamii.
Pia, ametoa shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi ya umeme ambayo imeendelea kuleta tija na mabadiliko chanya ya kimaendeleo nchini.
Kaimu Meneja wa TANESCO mkoani Singida, Mha. Boniface Shitindi, amebainisha kuwa kikao hicho kimeleta uelewa wa pamoja kuhusu gharama za kuunganishiwa umeme, matumizi ya mita janja, na umuhimu wa nishati safi ya kupikia.
Viongozi walioshiriki wameeleza kuridhishwa na elimu hiyo, wakiahidi kuifikisha kwa wananchi ili kulinda miundombinu na kutumia nishati hiyo kwa tija.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.