#HABARI: Wakazi wa Jiji la Arusha wamejitokeza kwa wingi katika kambi ya siku tatu iliyofanyika Hospitali ya St. Thomas ili kupatiwa huduma za uchunguzi na matibabu ya uhakika.

Kambi hiyo imewahusisha madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, macho, pamoja na meno, ambapo wananchi walionufaika wameeleza kufurahishwa na huduma hizo zilizolenga kutatua changamoto zao za kiafya.

Waratibu wa kambi hiyo, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Hospitali ya St. Thomas, Dkt. Kelvin Msuya pamoja na Dkt. Ebeneza Akyo, wameeleza kuwa lengo kuu la kambi hiyo ni kusogeza huduma za kibingwa karibu na jamii.

Kupitia kambi hii, hospitali hiyo imekusudia kuhakikisha wananchi wanapata matibabu ya hali ya juu kwa gharama nafuu na kusaidia kupunguza mzigo wa magonjwa yanayoweza kuzuilika kupitia uchunguzi wa mapema.

‎Powered by #MCHEZOSUPA
‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *