#HABARI: Waziri Mkuu Mh. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameweka jiwe la msingi la mradi mkubwa wa kupoza umeme katika eneo la Mkata mkoani Tanga.
Mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo chenye uwezo wa 2X60MVA pamoja na njia ya kusambaza umeme yenye urefu wa kilomita 45 kuelekea Kijiji cha Kwamsisi.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inagharamia mradi huu kwa jumla ya takriban Shilingi Bilioni 50.
Katika fedha hizo, Shilingi Bilioni 44.14 zimeelekezwa kwenye kituo cha kupoza umeme, huku Shilingi Bilioni 5.75 zikitumika kujenga miundombinu ya kusambaza nishati hiyo kwa wananchi.
Lengo kuu la uwekezaji huu ni kuimarisha Gridi ya Taifa ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika wilaya za Handeni na Kilindi.
Aidha, mradi utachochea ukuaji wa uchumi wa viwanda kwa kutoa nishati ya uhakika kwenye migodi ya Graphite iliyopo katika Kijiji cha Kwamsisi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioo