RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dk Patrice Motsepe, amewasili nchini asubuhi hi kwa ajili ya Mkutano wa Kamati Tendaji ya Shirikisho hilo.

Mutsepe amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Paul Makonda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, jijini Dar es Salaam.

Dk Motsepe ataongoza mkutano huo unaotarajiwa kufanyika leo, Dar es salaam.

Mkutano huo unatarajiwa kukutanisha viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika kwa ajili ya kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu.

Kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni ishara ya nafasi ya Tanzania katika ramani ya soka barani Afrika, hususan katika kipindi hiki cha maandalizi ya Fainali za Komba le Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *