HISPANIA: Kiungo wa zamani Arsenal, Thomas Partey, amefunguliwa mashtaka mawili ya ziada ya ubakaji yanayohusiana na madai ya tukio la ubakaji mwaka 2020 dhidi ya mwanamke mwingine.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Uingereza, Partey anatarajiwa kufikishwa mahakamani mwezi ujao kujibu tuhuma hizo.
Inaelezwa kuwa madai hayo yaliripotiwa kwa mara ya kwanza mwezi Agosti 2025, baada ya kuondoka Arsenal na kujiunga Villareal ya Hispania.
