Bihari ya Dawa (MSD), imeshinda tuzo ya Huduma kwa Wateja katika sekta ya Dawa na Vifaa Tiba inayotolewa na taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na kutoa mafunzo, vyeti na viwango vya taaluma ya huduma kwa wateja na vituo vya kupokea simu, Chartered Institute of Customer Management (CICM) Tanzania.

Tuzo hii inaonesha namna MSD ilivyoboresha huduma zake kwa wateja ikiwamo upatikanaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini.

MSD hadi sasa inahudumia vituo vya kutolea huduma za afya 8,893 nchi nzima, huku vituo vyote vikipelekewa bidhaa hizo hadi mlangoni mara sita kwa mwaka.

Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji, Hassan Ali amesema tangu kufanyika kwa maboresho Bohari ya Dawa, bidhaa za aina mbalimbali zimekuwa zikisambazwa kuendana na kasi ya uhitaji wa huduma hizo, ikiwemo mashine za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo, mashine za usingizi na hata zile za kuwezesha huduma za afya ya kinywa na meno ambazo huduma zote hutekelezwa kwa kuzingatia misingi ya huduma kwa wateja iliyowekwa.

Ameongeza kuwa MSD ina mifumo ya kisasa ya kuwasiliana na wateja kama vile Customer Portal, ujumbe wa simu (bulky sms), pamoja na Call Center ambapo zote hizi huwezesha kuwasiliana na wateja na kutatua changamoto mbalimbali.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *