#HABARI: Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, limepitisha Bajeti ya zaidi ya Shilingi Bilioni 57 kwa mwaka wa fedha ujao, huku shilingi Bilioni 12 za mapato ya ndani, sawa na asilimia 60, zikitengewa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Rasimu ya Bajeti hiyo iliwasilishwa na Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Bw. Christopher Masaaka, ambaye alieleza kuwa kipaumbele kitatolewa katika kukamilisha miradi viporo iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi, pamoja na kuendeleza miradi mipya itakayogusa sekta za elimu, afya, maji na miundombinu.
Amesema Halmashauri imejipanga kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, ili kufikia malengo iliyojiwekea, huku usimamizi madhubuti wa matumizi ya fedha ukizingatiwa ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana katika miradi inayotekelezwa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania