#HABARI: Kituo cha Huduma ya Simu kwa Mtoto (C-sema), kwa kushirikiana na UNFPA, kimeshiriki katika uzinduzi wa mpango mpya wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji na mila zilizopitwa na wakati nchini.

Mratibu wa miradi wa C-sema, Jeni Haule, amebainisha kuwa mpango huo unalenga kuelimisha jamii juu ya madhara ya ukeketaji na kuimarisha ulinzi wa haki za watoto wa kike na wanawake, ambao ndio waathirika wakuu wa vitendo hivyo vya ukatili.

Akizindua mpango huo shirikishi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima, amesisitiza kuwa serikali imejipanga kuwakamata wote wanaojihusisha na ukeketaji, wakiwemo mangariba na viongozi wa mila.

Mpango huu unaleta mkakati madhubuti wa kuunganisha nguvu za wadau na wananchi ili kuhakikisha watoto wa kike wanakuwa salama na mila kandamizi zinatokomezwa kabisa katika jamii.

.Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *