#HABARI: Maafisa 15 wa Jeshi la Polisi Tanzania mkoani Mbeya, wametunukiwa sifa na zawadi kwa mafanikio yao katika kuwanasa wahalifu hatari waliotekeleza makosa mbalimbali yaliyoigusa jamii, ikiwemo mauaji, ubakaji, pamoja na uuzaji na usafirishaji wa Dawa za Kulevya kama bangi, na miongoni mwa matukio yaliyotikisa jamii na kufanikiwa kufanyiwa kazi kwa ufanisi ni lile la kuuawa kwa mwanafunzi Shyrose Mabula, aliyekuwa akisoma katika Chuo Kikuu Mzumbe, Kitivo cha Sheria.
Askari hao wametunukiwa sifa na zawadi hizo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Familia, yaliyofanyika katika Uwanja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), yakilenga kutambua mchango wao katika kuimarisha usalama na amani ya wananchi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania