#HABARI: Matumizi ya majiko banifu yameleta tumaini jipya kwa wananchi kwa kuwezesha upikaji wa haraka, salama, na usio na moshi unaokera ambao ni hatari kwa afya na mazingira.

Teknolojia hii inasaidia kuweka hewa katika hali ya usafi, kutumia kuni kwa ufanisi mkubwa, na kupunguza muda unaotumika kuandaa chakula, jambo linalochochea ustawi wa familia.

Wananchi wa Kongwa wamekuwa mashahidi wa mabadiliko haya, wakieleza jinsi majiko hayo yalivyopunguza gharama za kuni na kulinda mazingira yao huku yakiboresha ladha ya mapishi.

Hatua hii inatajwa kuwa na matokeo makubwa katika kuboresha afya za watumiaji na kuimarisha maendeleo ya jamii kwa ujumla kupitia matumizi ya nishati safi.

.Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *