#HABARI: Mheshimiwa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi zake za Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education (GPE) na Mwenyekiti wa Bodi ya Global Water Partnership Southern Africa (GWPSA), ameshiriki katika Ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa African Union, uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia.
Katika mkutano huo wa ngazi ya juu, Rais Mstaafu alipata fursa ya kuonana na kufanya mazungumzo mafupi na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania.
Aidha, alikutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Nchi na Serikali waliopo madarakani, Wakuu wa Nchi Wastaafu wenzie pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Barani Afrika, wakijadiliana masuala ya maendeleo, elimu na rasilimali maji kwa mustakabali wa Bara la Afrika.
Ushiriki wake katika mkutano huo umeendeleza mchango wa Tanzania katika mijadala ya kimkakati inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda na maendeleo endelevu Barani Afrika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania