#HABARI: Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa onyo kwa Watanzania kutoruhusu ufa wa kubaguana kutokana na majukumu waliyonayo kwa kufanya hivyo kutaharibu nchi.

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo mkoani Tanga, huku akitahadharisha kwamba idadi ya watu inaongezeka kila siku, idadi ya mifugo inaongezeka lakini ardhi haiongezeki na kwamba suala la kupanga matumizi bora ya ardhi haliepukiki, “Tusiingize ufa wa kubaguana kwa kazi zetu, hiyo siyo nchi yetu tuliyoachiwa”

Amesema “Tunataka watu waishi wakiheshimu sheria, wakiitana ndugu, Tanzania ndiyo nchi tuliyoachiwa na wazee wetu, tuheshimu taratibu, huu utaratibu wa kiburi siyo asili ya nchi yetu, Serikali haiwezi kuvumilia watu wanaoishi kwa kiburi”, huku akisisitiza haja ya viongozi kuendelea kusisitiza amani na wananchi kuendelea kuitunza amani kwani mipango yote ya maendeleo inayopangwa haiwezi kutekelezwa kama hakuna amani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *