
Mkutano wa 39 wa Umoja wa Afrika unafunguliwa leo Jumamosi asubuhi, Februari 14, huko Addis Ababa, Ethiopia. Wakuu wa nchi na serikali zaidi ya hamsini wanashiriki. Wakati wa sherehe ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssouf, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, Mwenyekiti wa AU anayeondoka, João Lourenço wa Angola, na mrithi wake, rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, watahutubia hadhara kuu ya Umoja wa Afrika.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kutoka kwa mwandishi wetu maalum huko Addis Ababa, David Baché,
Kama kila mwaka, Rais wa Mamlaka ya Palestina na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia wataalikwa kuzungumza, pamoja na Giorgia Meloni, Rais wa Baraza la Mawaziri la Italia, ambaye yuko Addis Ababa kukuza uwekezaji wa Italia barani Afrika. Mkutano huu wa Umoja wa Afrika unakuja huku kukiwa na muktadha wa migogoro inayoongezeka na inayojikusanya. Masuala yaliyo mezani ni mengi na magumu kiasi kwamba maamuzi machache magumu yanatarajiwa.
Kuhusu mgogoro mashariki mwa DRC, michakato kadhaa tayari inaendelea: makubaliano ya Washington na Doha, maandalizi ya mazungumzo kati ya Wakongo, na pendekezo la kusitisha mapigano na mpatanishi wa Angola. Mkutano huo utahimiza hasa kuendelea kwa mipango hii.
Nchini Sudan, mgogoro unaoikabili nchi hii umekuwa wa kimataifa: Falme za Kiarabu wanatoa silaha, huku Chad na Ethiopia zikiruhusu silaha hizo kupita. Suala la uingiliaji kati huu wa nje litakuwa jambo nyeti. Vivyo hivyo kuingizwa tena kwa Sudan katika AU, kunakodaiwa na baadhi ya mataifa kuunga mkono serikali ya Jenerali Al-Burhan dhidi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vya Jenerali Hemedti. Lakini pendekezo hilo haliungwi mkono na baadhi ya nchi.
Ni chaguzi gani kwa Sudan Kusini?
Kuanza tena kwa mapigano nchini Sudan Kusini, kati ya jeshi linalomtii Rais Salva Kiir na SPLA-IO, vikosi vinavyomtii Makamu wa Rais wa zamani Riek Machar, ni suala ambalo pia litajadiliwa. Kushindwa kutambuliwa kwa Serikali ya umoja wa kitaifa kunaweza kusababisha AU kufikiria chaguzi zingine, lakini zipi?
Kuhusu Sahara Magharibi, Umoja wa Afrika bado haujachukua msimamo kuhusu mpango wa uhuru wa Morocco na mazungumzo yanayoendelea, chini ya usimamizi wa Marekani na Umoja wa Mataifa. Hili ni suala nyeti sana. Hali ni ngumu zaidi ikizingatiwa kwamba Sahara Magharibi ni sehemu ya Umoja wa Afrika, ingawa inatambuliwa na theluthi moja tu ya nchi wanachama—hali ya kipekee.
Burundi kushikilia urais wa kupokezana wa AU
Wakati wa mkutano huu, Angola itakabidhi urais wa kupokeza na kwa Burundi, ambayo rais wake, Evariste Ndayishimiye, ndiye mjumbe maalum wa AU kwa Sahel. Kwa kuwa nchi hizo tatu za ESA—Mali, Niger, na Burkina Faso—bado hazina mipango ya kufanya uchaguzi au kurudi katika utaratibu wa kikatiba, mkutano huo unaweza tu kudumisha vikwazo vyake kwa nchi hizi na kuhimiza upatanishi wa Burundi.
Nchini Guinea-Bissau na Madagascar, michakato ya mpito imeanzishwa kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya hivi karibuni. Wapatanishi walioagizwa na Umoja wa Afrika kwa nchi hizi watawasilisha ripoti zao kwa wakuu wa nchi na serikali, ambao kisha wataidhinisha rasmi muundo mpya wa Baraza la Amani na Usalama, kufuatia uchaguzi wa ngazi ya mawaziri uliofanyika mapema wiki hii. Katika chaguzi hizi, Benin, Gabon, Lesotho, Morocco, Somalia, na Afrika Kusini zilichaguliwa kama wanachama wapya. Côte d’Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sierra Leone, na Uganda zilichaguliwa tena.