Serikali imesema Kiwango cha utumikishwaji wa watoto nchini kimepungua kwa asilimia 9.1 kutoka asilimia 33.8 mwaka 2014 hadi asilimia 25.8 mwaka 2024.

Akizungumza kwenye Mkutano wa 6 wa Kimataifa wa Kutokomeza Utumikishwaji wa Mtoto (6th Global Conference on the Elimination of Child Labour), Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Rahma Kisuo amesema takwimu hizo zinatokana na ‘Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi’ uliofanyika mwaka 2024.

Mkutano huo ulioandaliwa na Shirika la Kazi Dunia (ILO) umewakutanisha mawaziri na wadau kutoka nchi 187 wanachama wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) wakiwemo wawakilishi wa serikali, mashirika na taasisi za umma, vyama vya wafanyakazi na wawakilishi wa vyama vya kijamii kwa lengo la kujadili na kukubaliana mikakati madhubuti ya kutokomeza utumikishwaji wa watoto ifikapo mwaka 2030.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF), ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika kuna zaidi ya watoto milioni 41 ambao wanatumikishwa na kukosa haki zao za utoto huku ikikadiriwa watoto milioni 138 duniani wanapitia hali hiyo.

Mkutano huo umefanyika katika jiji la Marrakech, Morocco kuanzia Februari 11 hadi Februari 13, 2026.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *