Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba ameagiza Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Tanga kufanya uchunguzi ili kubaini thamani ya fedha iliyotumika katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilindi kwa kuwa majengo yaliyojengwa ni machache kuliko yaliyokusudiwa.
Waiziri Mkuu Nchemba ametoa agizo hilo leo Jumamosi, Februari 14, 2026 akiweka jiwe la msingi la Hospitali hiyo iliyojengwa kwa gharama ya Sh2.64 bilioni ambapo kati ya fedha hizo Sh2.51 ni kutoka Serikali Kuu, Sh50milioni za mapato ya ndani ya Halmashauri na Sh89.9 milioni kutoka Benki ya Dunia (WB).
Pamoja na kuridhishwa na ubora wa majengo katika hospitali hiyo, Waziri Mkuu amemtaka Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga kufuatilia na kujua ni kwanini idadi ya majengo yaliyopo ni machache kuliko yaliyokusudiwa ikiwa fedha yote ya utekelezaji wa mradi ilitoka.
“Majengo yapo kwenye viwango vizuri, ila fedha iliyokuja ilikuwa ijenge majengo mengi zaidi lakini mmejenga pungufu, fedha nyingine zipo wapi?, michezo ya upotevu wa fedha za Serikali hatuwezi vumilia” amesisitiza Waiziri Mkuu Nchemba.
(Feed generated with FetchRSS)