
MOROCCO; AZAM imemaliza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa na pointi tisa, lakini imekwama kutinga robo fainali.
Azam leo imepoteza mchezo wake wa mwisho hatua ya makundi kwa kufungwa mabao 2-0 na Wydad nchini Morocco, ambapo sasa Wydad imemaliza kinara kundi hilo ikiwa na pointi 15, ikifuatiwa na AS Maniema Union yenye pointi 12 baada ya leo kuifunga Nairobi United mabao 3-0.

Azam imemaliza ya tatu katika Kundi B ikiwa na pointi 12 na Nairobi United yenyewe imemaliza ya mwisho kwenye kundi hilo bila pointi.