
Ugonjwa wa kipindupindu unaenea ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kufikia gereza kubwa zaidi nchini humo la Makala, jijini Kinshasa. Vifo vimeripotiwa katika gereza hilo. Wagonjwa kadhaa wamethibitishwa miongoni mwa wafungwa. Mamlaka ya mahakama imetangaza hatua za dharura kujaribu kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Pascal Mulegwa
Waziri wa Sheria anatoa tahadhari. Mlipuko wa kipindupindu sasa unaripotiwa katika gereza kubwa zaidi nchini DRC. Gereza Kuu la Makala, lililojengwa na kupokea wafungwa 1,500, kwa sasa lina wafungwa karibu mara nane ya idadi hiyo. Msongamano huu unachochea kuenea kwa magonjwa yanayosababishwa na maji. Katika hatua hii, wagonjwa kumi na tatu walioambukizwa virusi vya ugonjwa huo mamethibitishwa. Wafungwa wanne wamepona.
Wagonjwa wengine kumi na tano wanaoshukiwa pia memeripotiwa na huduma za afya. Ili kuepuka hali nzito, mamlaka zinachukua hatua za kipekee. Kulazwa kwa wafungwa wapya ni marufuku hadi taarifa zaidi itakapotolewa, na watu kutembelea ndugu au jamaa zao katika jela hilo kumesitishwa au kupunguzwa sana, kwa kuheshimu na kufuata itifaki za usafi.
Idadi ya wauguzi imeongezwa
Mwitikio ulioimarishwa wa kimatibabu umetangazwa, ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwa timu za afya, utoaji wa dawa muhimu, dawa za kuua vijidudu, na vifaa vya kinga.
Tahadhari hii inakuja huku kukiwa na hali ya kiafya ambayo tayari inatia wasiwasi nchini DRC. Nchi hii inakabiliwa na magonjwa kadhaa ya mlipuko kwa wakati mmoja: kuenea kwa Mpox, kuendelea kwa kipindupindu, na mlipuko wa surua.
Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Umma, kiwango cha vifo kutokana na kipindupindu kimefikia 4.37% katika maeneo yasiyo na ugonjwa. Wizara ya Afya inaelezea kwamba kuwasili kwa wagonjwa kwa kuchelewa, mara nyingi wakiwa katika hali ya upungufu mkubwa wa maji mwilini, ni sababu ya kuogezeka kwa vifo hivyo.