#HABARI: Kupitia mitandao ya kijamii kulisambazwa picha mjongeo akionekana mtoto mdogo wa kiume na zikisikika sauti zikimhamasisha kuvuta sigara, Jeshi la Polisi limesema, kitendo hicho ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za kijamii na nchi.

Jeshi la Polisi, limeanza uchunguzi na kuwafuatilia watu hao kwa hatua nyingine za kisheria.

Aidha, linatoa wito kwa yeyote anayewafahamu watu hao au mtoto huyo asaidie kuwafikia na kuokoa afya ya mtoto huyo.

Pia, linatoa onyo kwa watu wenye tabia za kufanya vitendo vya kikatili na vya unyanyasaji kama hivyo na vinavyofanana na hivyo kwa watoto kwa lengo lolote lile ikiwepo msukumo wa kutafuta wafuasi (followers) kwa ajili ya mitandao yao ya kijamii kuziacha kwani halitasita kuwakamata kwa sababu ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za nchi.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *