#HABARI: Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imesababisha maafa makubwa katika kata za Isanga na Iganzo jijini Mbeya baada ya kubomoa na kuezua mapaa ya nyumba 34, yakiwemo makanisa mawili.
Janga hilo limeziacha kaya hizo bila mahali pa kuishi, huku likisababisha hasara kubwa ya uharibifu wa samani za ndani, mazao mashambani pamoja na simanzi kwa wakazi wa maeneo hayo.
Viongozi wa Serikali ngazi ya Kata, wakiongozwa na Diwani wa Iganzo, Mhe. Daniel Mwanjoka, na Diwani wa Viti Maalum, Mhe. Atu Msai, wamewatembelea waathiriwa na kutoa tathmini ya awali ya uharibifu huo huku mvua zikiendelea kunyesha.
Waathiriwa, akiwemo Bw. Albart Sanga na Bw. Patrick Sungura, wameiomba Serikali na wadau wa maendeleo kuwapatia misaada ya hali na mali ili waweze kurejea katika makazi yao na kukabiliana na hali ngumu waliyoipata.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.