#HABARI: Taasisi ya Ukaguzi na Udhibiti wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imefanya operesheni ya kushtukiza mkoani Singida na kubaini baadhi ya wamiliki wa maduka ya pembejeo wakihujumu mfumo wa ruzuku kwa kuskani mbegu na kuziuza kwa bei ya juu kinyume na taratibu.

Mkaguzi wa TOSCI, Dkt. Levini Msimbira, ametoa onyo kali kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wakiukaji hao, huku baadhi ya wafanyabiashara wakikiri kuhusika na vitendo hivyo vinavyokwamisha malengo ya Serikali ya kumsaidia mkulima.

Hatua hiyo imepongezwa na wakulima pamoja na wadau wa kilimo mkoani humo, wakieleza kuwa ukaguzi huo ni mkombozi katika kuhakikisha mbegu bora zinawafikia walengwa kwa bei elekezi.

Afisa Kilimo wa Mkoa, Bw. Lucas Mkuki, amesisitiza umuhimu wa uaminifu katika usambazaji wa pembejeo, huku TOSCI ikiahidi kuendeleza operesheni hizo ili kumlinda mkulima dhidi ya unyonyaji na kuhakikisha usalama wa chakula nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *