#HABARI: Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Mtwara imepata mafanikio makubwa kupitia miradi saba ya mita za malipo ya kabla (pre-paid meters) inayohudumia vijiji 11.
Mhandisi Alois Milyangula ameeleza kuwa teknolojia hiyo imeongeza makusanyo ya mapato kwa asilimia 40 na kupunguza kwa kiasi kikubwa upotevu wa maji, huku mradi huo ukifadhiliwa na Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB) kupitia ufungaji wa vichoteo 38 katika maeneo ya walengwa.
Wananchi wa Kata ya Kilambo wamepongeza mfumo huo mpya wakisema umemaliza migogoro ya usambazaji wa maji na kuimarisha ufanisi katika shughuli zao za maendeleo.
Wasimamizi wa vizimba vya maji, wakiongozwa na Ketty Nambole, wamebainisha kuwa mita hizo zinawawezesha wananchi kupata huduma kulingana na uwezo wao wa kifedha, jambo lililoondoa usumbufu uliokuwepo awali na kuhakikisha huduma ya maji inakuwa endelevu na yenye uhakika kwa jamii.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.