.

Chanzo cha picha, Reuters

Tehran Iran iko tayari kufikiria maafikiano ili kufikia makubaliano ya nyuklia na Marekani ikiwa Wamarekani watakuwa tayari kujadili kuondoa vikwazo, waziri wa Iran ameiambia BBC.

Maafisa wa Marekani wamesisitiza mara kwa mara kwamba Iran, sio Marekani, inashikilia maendeleo katika mchakato huu wa muda mrefu wa mazungumzo.

Siku ya Jumamosi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema Rais Donald Trump anapendelea makubaliano lakini ni vigumu “kufikia malengo hayo ” na Iran.

Lakini katika mahojiano na BBC mjini Tehran, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Majid Takht-Ravanchi, alisema mpira uko kwenye katika mikono ya Marekani ili kuthibitisha kwamba wanataka kufanya makubaliano, na kuongeza: “Ikiwa ni waaminifu, nina uhakika tutakuwa njiani kufikia makubaliano.”

Trump ametishia kuishambulia Iran ikiwa makubaliano ya kuzuia mpango wake wa nyuklia hayatafikiwa, huku Marekani ikiimarisha uwepo wake wa kijeshi katika eneo hilo.

Hii inafuatia ukandamizaji mkali wa Iran wa maandamano ya nchi nzima dhidi ya serikali mwezi uliopita, ambayo mashirika ya haki za binadamu yanasema yaliua maelfu ya watu.

Marekani na Iran zilifanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja katika jimbo la Ghuba la Oman mapema mwezi wa Februari, na Takht-Ravanchi, ambaye alithibitisha kuwa duru ya pili ilikuwa ifanyike Geneva siku ya Jumanne, alisema walikuwa “zaidi au kidogo katika mwelekeo mzuri lakini ni mapema mno kuhukumu”. Trump pia ameelezea mazungumzo hayo kuwa mazuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *