Jamii imetakiwa kuongeza uelewa na kubadili mtazamo kuhusu watu wenye ulemavu, kufuatia kuendelea kuwepo kwa vitendo vya unyanyapaa na ubaguzi vinavyotokana na elimu duni ya kuwajali na kuwaheshimu kama sehemu ya jamii.
Katika mazingira mengi, watu wenye ulemavu bado hukumbana na dhana potofu zinazowachukulia kuwa hawana mchango wala faida katika jamii, au hawafai kuanzisha familia na mahusiano ya kawaida. Mitazamo hiyo imeendelea kuathiri haki zao za msingi na kuwanyima fursa sawa za kijamii na kiuchumi.
Mkurugenzi wa Tupo Sawa Organization, Jackline Bakari Mtaita, amesema ingawa elimu kuhusu haki za watu wenye ulemavu imekuwa ikitolewa, bado uelewa wa kina wa kuwajali na kuwachukulia kama watu wa kawaida haujafikiwa ipasavyo
✍Ibrahimu Kilumbo
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)