Katika jitahada za kuungana mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu nchini, Wadau, viongozi na watumishi wote waliowahi kusoma katika Shule ya sekondari ya Minaki iliyopo Kisarawe Pwani wamepewa wito wa kujitokeza kushiriki jitahada za kukabati miundo ya shule hiyo yenye zaidi ya miaka 100.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Dkt Seleman Jaffo ambaye pia ni miongoni mwa wanafunzi waliosoma katika shule hiyo, wakati akijibu kuhusu changamoto za uchakavu wa baadhi ya majengo, ukosevu wa gari la dharura kwa wagonjwa na uhaba wa kompyuta kwa ajili ya masomo ya tehama shuleni hapo zilizowasilishwa kwake akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya 66 ya kidato cha sita.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *