Katika Kusuma mbele agenda ya serikali ya kuhakikisha ifikapo 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia wadau wameendelea kuunga mkono kwa kubuni mbinu mbalimbali za kuwahamasisha watanzania kutumia nishati hiyo.

Wakizungumza Jijini Dar es salaam ikiwa ni namna ya kuadhimisha siku ya wapendanao Duniani Kampuni ya Total Energies na Hisense zimezindua kampeni inayolenga kuwapatia ofa ya mtungi wa gesi wateja wanaonunua Jiko la Hisense lengo ni kuwapa fursa hiyo watanzania waweze kuhama kutoka matumizi ya nishati isiyo safi na kuingia kwenye teknolojia ya kisasa.

Ofa hiyo ambayo inaanza leo hadi April haijawaacha nyuma watanzania katika msimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na Mfungo wa Kwaresma ambao unahusisha Zaidi masuala ya mapishi ambayo yanategemea matumizi ya nishati safi ili kulinda afya za wapishi na walaji.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *