Serikali ya Madagascar jana ilitangaza kwa kimbunga cha Gezani kilichoiathiri nchi hiyo ni janga la kitaifa. Kimbunga hicho cha kitropiki kmesasabisha vifo vya 43, majeruhi kadhaa, uharibifu wa miundombinu na makazi, na hasara kubwa katika baadhi ya maeneo.

Waziri Mkuu wa Madagascar Rajaonarivelo Heritsalama amesema akiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Antananarivo kwamba kimbunga hicho kimeathiri uchumi wa nchi na maisha ya watu. Amesema serikali itajikita katika kuimarisha ustahimilivu ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika siku zijazo.

Kulingana na takwimu zilizotolewa Jumamosi na Idara ya Kukabiliana na Maafa na Majanga ya Kimaumbile ya Madagascar, kimbunga hicho kimeisababisha vifo vya watu 43 katika wilaya 25 katika mikoa mitano ya nchi hiyo. Aidha  watu 427 wamejeruhiwa na sita hawajulikani walipo. 

Idara ya Kukabiliana na Maafa na Majanga ya Kimaumbile ya Madagascar imeeleza kuwa nyumba 357,014 zimeharibiwa, watu 16,428 wamelazimika kuhama makazi yao na majengo 42,219 yamebomolewa.

adagascar ni kati ya nchi  ambazo mara kw amara zinaathiriwa na vimbunga barani Afrika na bado inakabiliwa na athari za Kimbunga cha cha Kitropiki kwa jina la  Fytia, kilichopiga wiki mbili zilizopita na kuua watu saba na kuathiri zaidi ya wengine 54,000.

Kimbunga kikali cha Kitropiki cha Gezani kiliathiri maeneo ya mashariki mwa Madagaska  tarehe 10 mwezi huu wa Februari, kikiwa na upepo wa kasi ya takriban kilomita 180 kwa saa na mawimbi yaliyokuwa yakizidi kasi ya kilomita 230 kwa saa. Bandari ya Toamasina iliathirika zaidi, ambapo uharibifu mkubwa wa majengo na miundombinu umeripotiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *