Madhehebu ya Dini ya Kiislamu yanayofanya kazi chini ya taasisi mbalimbali yameaswa kuendelea kuishi kwa kuzingatia misingi na malengo ya kuanzishwa kwake, sambamba na kudumisha umoja na mshikamano ili kulinda na kuendeleza amani ya nchi.
Wito huo umetolewa jijini Arusha wakati wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Taasisi ya Fiysabilillah Tabligh Markaz, uliowakutanisha waumini kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania Bara, Zanzibar, Kenya, Uganda na Malawi.
Akizungumza katika mkutano huo, Sheikh wa Mkoa wa Arusha, Shabani Juma, amesema tofauti za kimadhehebu ni jambo la kawaida ndani ya Uislamu, lakini hazipaswi kuwa chanzo cha migawanyiko.
✍ Ramadhani Mvungi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)