Wakati usitishaji mapigano ukitarajiwa kuanza siku ya Jumatano, Februari 18, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mapigano makali yanayoambatana na mashambulizi ya mabomu yanaendelea katika nyanda za juu za Minembwe, katika eneo la Fizi katika mkoa wa Kivu Kusini, kati ya wapiganaji wa Twirwaneho—wanaoshirikiana na AFC/M23—na jeshi la Kongo, linaloungwa mkono na jeshi la Burundi na wanamgambo wa Wazalendo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mapigano yanaendelea licha ya wito wa Marekani siku ya Jumamosi, Februari 14, wa kukomesha uhasama. RFI iliweza kuwasiliana na Mufashe Santos, kiongozi wa shirika la kiraia la Minembwe, eneo ambalo huduma ya mawasiliano imezimwachini kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Mufashe Santos anasimulia mateso ya kila siku yanayowakabili wakazi wa eneo hili lililotengwa, kufuatia mapigano yanayoendelea.

Hali hii inakuja wakati mkuu wa MONUSCO, Vivian Van de Perre, akiwa katika shughuli za kikazi katika mji wa Goma, ambapo amekutana na mamlaka ya AFC/M23 na Mfumo wa Uthibitishaji wa Pamoja Uliopanuliwa (EJVM).

“Bado tunapigwa mabomu na ndege zisizo na rubani za serikali. Karibu kila kitu kinaonyesha kwamba mapigano yanaendelea. Bado wanashambulia, na bado kuna waathiriwa. Tumeomba mara kwa mara kuwepo na maeneo ya kibinadamu. Sasa ningependa kuelekeza maneneo yangu kwa Umoja wa Afrika. Wakazi wa Nyanda za Juu wanaendelea kushambuliwa kwa mabomu na kuuawa. Mashambulizi hayo yanafanyika mchana na usiku. Mabomu haya ya ndege zisizo na rubani yanalenga nyumba za raia. Huduma ya mawasiliano imezimwa, na hili ni jambo la dharura kweli…” “Tulikuwa tukifanya biashara kwa simu, lakini leo watu wa Minembwe hawana tena njia ya kuishi,” anasema Mufashe Santos, mkuu wa mashirika ya kiraia huko Minembwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *