Watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki wamevamia vijiji vitatu kaskazini mwa Nigeria, na kuua takriban watu 32 na kuwateka nyara wengine kadhaa.

Mashambulizi hayo yameripotiwa jana katika eneo la Borgu katika jimbo la Niger huku kukiwa na tatizo kubwa la usalama kaskazini mwa Nigeria, likiyahusisha na makundi ya wanamgambo wenye silaha yenye mfungamano na kundi la ISIS au Daesh na pia magenge mengine ya uhalifu yanayowateka nyara watu ili kupewa mlungura.

Wasiu Abiodun Msemaji wa Polisi wa jimbo la Niger kaskazini mwa Nigeria amethibitisha kujiri shambulio katika kijiji kimoja. Amesema, watu wanaoshukiwa kuwa majambazi walishambulia kijiji cha Tunga-Makeri na kuuwa watu sita.

Majambazi hao aidha walichoma moto nyumba kadhaa na hadi sasa haijafahamika ni raia wangapi waliotekwa nyara katika shambulio hilo.

Baada ya kufanyauhalifu katika kijiji cha Tunga-Makeri; watu hao wenye silaha walielekea katika kijiji cha Konkoso. Jeremiah Timothy mkazi wa kijiji cha Konkoso ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanamgambo wenye silaha walikivamia kijiji chao mapeam jana huku wakifyatua ovyo risasi.

Mkazi mwingine wa kijiji cha Konkoso amesema: Watu wasiopungua 26 wameuwa hadi sasa katika kijiji hicho baada ya watu  wenye silaha kukichoma moto kituo cha polisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *