
Abiy Ahmed Waziri Mkuu wa Ethiopia amehimiza kuhusu ushirikiano mpya kati ya Afrika na Ulaya unaozingatia utu na ustawi wa pamoja. Waziri Mkuu wa Ethiopia ameeleza haya alipokuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Italia na Afrika mjini Addis Ababa mji mkuu wa nchi hiyo.
“Kwa pamoja, tunaweza kujenga uhusiano mpya wa Afrika na Ulaya, usio tegemeza, bali uliojengeka katika misingi ya utu; si kwa kwa ajili ya ustawi wa pamoja,” amesema Abiy Ahmed.
Mwenyekiti mwenza wa mkutano huo wa Addis Ababa, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni kwa upande wake amesema kuwa ushirikiano wa Italia na Afrika “unategemea manufaa ya pande zote na utaendelea kuimarika,” na kwamba “Mpango wa Mattei” wa Roma unakusudia kuwanufaisha pakubwa watu wa Afrika.”
Lengo la Mpango wa Mattei ambao ulianzishwa mwaka 2024 baada ya mkutano wa kwanza wa Italia na Afrika kufanyika Rome mapema mwaka huo ni kukuza ushirikiano unategemea uwekezaji katika nishati, miundombinu, kilimo na utoaji mafunzo.
Italia imesema kuwa ubunifu huo umedhamimia kuchochea maendeleo na kusaidia kuzuia uhamiaji usio wa kawaida kwa kusaidia miradi ya pamoja.
Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye alishiriki mkutano huo ameeeleza kuwa: Ushirikiano ni lazima ujengwa kwa misingi ya kuheshimiana na kuaminiana. Aidha ametaka kufanyiwa marekebisho mifumo ya fedha kimataifa ili kuziba pengo la kuziba pengo la ufadhili wa maendeleo la dola trilioni 4 kwa mwaka na kupunguza gharama kubwa za kukopa zinazokabili nchi za Afrika.
Viongozi kutoka barani Afrika na Ulaya, wakiwemo maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika wamehudhuria mkutano huo ulioangazia nishati, mabadiliko ya tabianchi, mageuzi ya kidijitali na maendeleo ya viwanda.