Nchini Ethiopia, wakati mvutano huko Tigray ukiongezeka, serikali ya shirikisho inapoteza nguvu katika eneo la Amhara. Katika vita na serikali kwa miaka mitatu, waasi katika eneo la Amhara, pia wanajulikana kama Fano, wanapata tena nguvu na kudhibiti baadhi ya maeneo. Miji muhimu imetekwa tena, ikiwa ni pamoja na Debre Tabor, yapata kilomita 100 kutoka mji mkuu wa eneo hilo. Ndege zisizo na rubani zilishambulia mji huo mara kadhaa wiki iliyopita.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo wa Amhara wanapokea usaidizi wa kijasusi na vifaa kutoka kwa waasi wa Tigray na Eritrea, kulingana na ofisi ya amani na usalama ya eneo la Amhara, ambayo ni sehemu ya serikali ya shirikisho. Wanamgambo katika eneo la Amhara, pia wanajulikana kama Fano, wamechukua tena udhbiti wa miji ya kimkakati. Mamlaka ya shirikisho inahusisha hili na ushirikiano kati ya makundi mbalimbali ya waasi.

Waasi wa Amhara na Tigray walikuwa mahasimu wakati wa vita vya Tigray kati ya mwaka 2021 na 2022, lakini maslahi yao sasa yanaungana katika mapambano yao dhidi ya serikali ya shirikisho. Kulingana na wachambuzi kadhaa, miungano hii ipo, ingawa kwa njia ya kimazingira na ya ndani. Hata hivyo, wanamgambo bado wamegawanyika na wanaratibiwa vibaya.

Kusonga mbele kwa waasi katika eneo la Amhara pia kuliwezeshwa na kuondolewa kwa wanajeshi wa shirikisho, ambao walihamishiwa Tigray. Kwa upande wake, kiongozi wa kundi la waasi ya Tigray People’s Liberation Front (TPLF) anakanusha madai haya. Kulingana na kiongozi huyo wa waasi, serikali inajiandaa kwa vita vikubwa katika eneo hilo. Leo, kiongozi wa kundi hilo ameongeza tena wito wake kwa jumuiya ya kimataifa, akisema kwamba “hatasimama bila kufanya chochote” ikiwa makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka wa 2022 hayataheshimiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *