#HABARI: Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Delilah Kimambo, amekutana na Prof. David Prologo kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory kwa ajili ya kuanza kambi maalumu ya tiba ya maumivu bila upasuaji.
Kambi hiyo ya wiki moja, inayoanza Februari 16 hadi 20, 2026, inatumia teknolojia ya kisasa ya Tiba Radiolojia (Image-Guided) kutoa matibabu ya kibobezi kwa wagonjwa wenye maumivu makali ya viungo, uti wa mgongo, na neva.
Huduma hizi zinawalenga zaidi wagonjwa wenye maumivu sugu ya magoti, nyonga, na saratani ambao hawajapata nafuu kwa matibabu mengine, pamoja na wale waliovunjika pingili za uti wa mgongo.
Aidha, ushirikiano huu unalenga kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani wa Muhimbili ili kuimarisha na kupanua upatikanaji wa huduma hizi za kisasa za tiba ya maumivu nchini Tanzania.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.