#HABARI: Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Festo Dugange, amezitaka ofisi za pande zote mbili za Muungano kulipa kipaumbele suala la Uchumi wa Buluu katika vikao vyao vya ushirikiano.

Akizungumza visiwani Zanzibar leo Februari 16, 2026, Dkt. Dugange amebainisha kuwa kuimarisha ushirikiano katika sekta hiyo kutaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa na kutoa uelewa zaidi kwa wananchi kupitia kitengo kipya cha usimamizi wa Uchumi wa Buluu kilichoanzishwa.

Dkt. Dugange amesisitiza umuhimu wa kuelezea fursa lukuki zinazotokana na Muungano, ikiwemo miradi ya biashara ya kaboni na maendeleo ya mazingira, badala ya kujikita kwenye changamoto pekee.

Amewapongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa juhudi zao za kuimarisha miundombinu na huduma za kijamii, hatua ambazo zimekuwa chachu ya kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali zao zote mbili.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Hamza Hassan Juma, ameshauri kutumiwa kwa wasanii na vijana katika kutoa elimu ya Muungano ili ujumbe ufike kwa haraka na ufanisi zaidi.

Amewataka watendaji kutangaza fursa zilizopo na kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali zinaendelea kuzifanyia kazi changamoto zilizosalia, huku akipongeza uimara wa uchumi wa Tanzania unaozidi kukua siku hadi siku.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *