#HABARI: Polisi nchini Nigeria wamesema wamewakamata washukiwa wanne wa utekaji nyara wa watoto tisa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu John, waliokuwa wakisali kanisani hapo, eneo la Serikali ya Mtaa ya Ado Jimbo la Benue Februari 08, 2026.

Mshauri wa Gavana wa Jimbo la Benue Solomon Lorpev, ametoa taarifa akisema watoto hao waliokolewa jumla ni wasichana sita na wavulana watatu, ambao wanaendelea kupewa matibabu.

Kumekuwa na matukio mengi ya utekaji nyara nchini Nigeria na kusababisha uchunguzi wa Kimataifa, hasa kutoka Marekani, juu ya hali mbaya ya usalama katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Benue ni sehemu ya eneo linaloitwa Ukanda wa Kati nchini Nigeria, ambalo limeshuhudia mapigano kati ya wakulima na wafugaji kuhusu ardhi na maliasili, pamoja na utekaji nyara unaofanywa na wahalifu wenye silaha.

Kufuatia utekaji nyara huo, Rais wa Nigeria Bola Tinubu alitangaza hali ya hatari mnamo mwezi Novemba na kuanzisha zoezi la kuwaajiri wanajeshi na polisi zaidi.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *