#HABARI:Madiwani katika Jimbo la Busanda Mkoani Geita wameunganisha nguvu kufanya ukarabati wa dharura wa barabara zinazounganisha kata zao ili kunusuru hali ya usafiri na usafirishaji wa mazao kutoka mashambani wakati wakiendelea kungoja bajeti ya serikali ya ukarabati wa barabara hizo.
Madiwani wa kata ya Nyarugusu Mheshimiwa Samata Makula na kata ya Nyaluyeye Mheshimiwa Mohamed Lyagaba wamesema wanajisikia fahari kuwa mfano kwa kuhakikisha wanachangishana fedha za kugharamia ukarabati huo unaowezesha wananchi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao bila vikwazo wakati wakingoja fedha kutoka serikalini kwa ajili ya kukarabati barabara hizo.
Akiongea na Waandishi wa habari Mbunge wa Jimbo la Busanda ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Dkt. Jafar Saif amesema wamechukua hatua hiyo ya dharura ili kuhakikisha wanaimarisha mawasiliano kupitia barabara ili kunusuru shughuli za kiuchumi zisikwame wakati wakiendelea kungoja Bajeti ya serikali iliyotengwa kwa ajili ya kufanya ukarabati wa baadhi ya barabara katika jimbo hilo.
Barabara hiyo ya Bukoli kwenda Muhama hadi Nyarugusu ni barabara inayopita katika mashamba ya viazi na mihogo ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga kuwasaidia wakulima kusafirisha mazao yao kutoka shambani na kuyafikisha maeneo yenye usafiri wa uhakika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.