Nchini BurkinaFaso, mji wa Titao, ambao hapo awali uliokolewa kutokana na mashambulio ya kigaidi, ulivamiwa na kundi la washambuliaji siku ya Jumamosi, Februari 14, 2026. Walishambulia na kupora kambi ya kijeshi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mashahidi waliripoti kwamba waasi walichoma moto soko la mji huo na kuharibu miundombinu ya mawasiliano ya simu.

Msemaji wa vikosi vya jeshi, Luteni Kanali Abdoul Aziz Ouedraogo, alithibitisha shambulio hilo Jumapili jioni, Februari 15, kwenye televisheni ya kitaifa.

Akizungumza kwenye runinga ya taifa  Abdoul Aziz Ouedraogo, amesema hali imedhibitiwa huku akithibitisha kwamba “mashambulizi mengi” yalifanyika Jumamosi kaskazini mwa nchi, huku akisifu “ushujaa na weledi wa vikosi vya ulinzi ambavyo vilikuwa vimewashinda magaidi hao kwa kuwazuia kuwaangamiza.”

Kulingana na vyanzo vya ndani, washambuliaji hao walikuwa “wengi sana.” Waligawanywa katika makundi matatu. La kwanza, lililoundwa na wanaume wenye silaha kwenye pikipiki, lilivamia kambi ya kijeshi, likipora silaha na risasi.

Kundi la pili la washambuliaji liliharibu mitambo ya simu, na kuutenga mji wa Titao. Hatimaye, kikosi cha tatu kiliingia mjini na kuvamia soko. Waasi hao walipora na kisha kuchoma moto maduka na malori ya usambazaji.

Baada ya shambulio hilo, inasemekana walielekea kaskazini tena. Huku wakiahidi kurejea tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *