
Nchini Kenya, mpasuko wa kisiasa ndani ya chama cha siasa cha ODM umeendelea ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita, pande mbili zinazovutana kuhusu kumuunga mkono rais William Ruto, ziliandaa mikutano ya hadhara.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jijini Mombasa kiongozi wa chama Oburu Oginga, alikutana na wafuasi wa chama hicho, na kusisitiza sababu ya kumwondoa kwenye nafasi ya Ukatibu Mkuu Edwin Sifuna.
‘‘Hata kama mimi nikikosa nidhamu niondolewe, yule Katibu Mkuu mwengine chama kilisema akae nje kidogo kwa sababu ya kukosa nidhamu.’’ Alisema Oburu Odinga.
Oburu Odinga- Kiongozi wa ODM
Kwa upande wake, Sifuna ambaye Mahakama ilizuia kuondolewa kwake kwenye nafasi hiyo, aliongoza mkutano wa maelfu ya wafuasi wake mjini Kitengela, katika Kaunti ya Kajiado, na kusisitiza ataendelea kuukosoa utawala wa rais Ruto.
‘‘Tutaendelea kuongea ukweli ilituweze kulinda wanachi wetu kutokana na dhuluma za Rais Ruto na ufisadi ambao umekithiri kwenye nchi hii.’’ Alieleza Sifuna.
Edwin Sifuna – Aliyekuwa Katibu Mkuu wa ODM
Mpasuko ndani ya chama cha ODM, umeibuka baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi wake Raila Odinga aliyefariki dunia mwaka uliopita, lakini pia viongozi wa waandamizi kutofautiana kuhusu kumuunga mkono rais Ruto wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.