Mashine za kukatia majani ya mifugo ni vifaa hatari vyenye visu vikubwa vya mviringo vinavyozunguka kwa kasi kubwa, vikichochewa na jenereta ndogo. Zikitumiwa na wafanyakazi wa vijijini katika nchi kadhaa zinazoendelea, zikiwemo India, Pakistan na Kenya, mashine hizi hubeba hatari ya kudumu wengi wamekatwa vidole au mikono yao kufuatia ajali.

Athari zake ni za kusikitisha. Shughuli za kila siku zinazounda maisha kama kuvuna mazao, kukanda unga, kushona urembo wa mikono ghafla huwa haziwezekani. Maelfu ya wanawake hubaki na uhuru mdogo, kupoteza riziki zao, na mara nyingi hukumbwa na kutengwa kijamii.

Mwanamke wa eneo la vijijini la Pakistan aliyejeruhiwa na mkataji wa chakula.

Mwanamke wa eneo la vijijini la Pakistan aliyejeruhiwa na mkataji wa chakula.

Hadi hivi karibuni, viungo bandia vya kisasa vilikuwa mbali kabisa na uwezo wao wa kuvipata. Sasa, zana za AI zilizobuniwa ndani ya nchi zao zinafungua milango ya kupata vifaa vya hali ya juu kama vinavyopatikana katika nchi tajiri.

Kampuni ya Bioniks Technologies yenye makao yake makuu mjini Karachi Pakistan ilishirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake UN Women, kubuni na kusambaza viungo bandia vilivyoundwa mahsusi kwa wafanyakazi wanawake walioathirika katika jimbo la Sindh nchini Pakistan. Mpango huo umetumia teknolojia za kisasa za uundaji wa miundo ya 3D, uchunguzi wa kidijitali, na akili bandi kutengeneza mikono ya kibiolojia iliyo mwepesi, imara na rahisi kutumia, inayoweza kubadilisha maisha ya kila siku.

“Kupitia ushirikiano huu, tumetengeneza mikono ya kisasa ya bandia, mafunzo ya vitendo, msaada wa kisaikolojia na vikao vya uhamasishaji kusaidia jamii kuelewa kanuni za usalama na kuzuia majeraha kama haya siku zijazo,” anasema Ayesha Zulfiqar, mwanzilishi mwenza wa Bioniks.

Ameongeza kuwa “Kuona wanawake hawa jasiri wakirejesha uwezo wao wa kusonga mbele, heshima, uhuru na kurejea kwenye ushonaji wa mikono chanzo chao kikuu cha mapato limekuwa jambo la kutia moyo sana. Hii si teknolojia tu, ni kurejesha matumaini, kujiamini na fursa.”

Bendera kubwa ya rangi ya zambarau kwenye kituo cha basi jijini New Delhi inawakaribisha wajumbe wa Mkutano wa Athari za AI, uliopangwa kufanyika Februari 18-20, 2022, katika Uwanja wa Taifa.

© UN News/Anshu Sharma

Mkutano wa AI Impact 2026, mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu akili Mnemba ambao utafanyika Global South kwa mara ya kwanza kwa kiwango hiki.

Mkutano wa AI India: Hatua ya kwanza Kusini mwa Dunia

Mpango huu ni mfano thabiti wa kile kinachoweza kufikiwa wakati AI inapatikana kwa wabunifu wa Kusini mwa Dunia.

Kutoa demokrasia kwa AI ni kipaumbele kikubwa cha Umoja wa Mataifa, unaojitahidi kuhakikisha kuwa teknolojia hii inayokua kwa kasi inatengenezwa kwa misingi ya maadili na kuwanufaisha watu kila mahali.

Katika Mkutano wa India wa Athari za AI unaofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 20 Februari mjini New Delhi, mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa yataonesha miradi wanayoiunga mkono nchini humo na katika nchi zinazoendelea.

Mkutano huo ni wa kwanza mkubwa wa aina yake katika ukanda wa Kusini mwa Dunia. Ukijengea juu ya msukumo wa Mkutano wa Usalama wa AI wa mwaka 2023 ulioitishwa na Uingereza, na Mkutano wa Hatua za AI wa 2025 nchini Ufaransa, pia utamshirikisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres pamoja na mjumbe wake maalum wa Teknolojia za Kidijitali na Zinazochipukia, Amandeep Gill.

Akizungumza na mwandishi na mtangazaji wa podikasti Anirudh Suri kabla ya mkutano, Bwana. Gill amesema kuwa Umoja wa Mataifa umejikita katika kuziba pengo linalokua la AI kati ya uchumi tajiri na wa nchi zinazoendelea, na pia kati ya matajiri na maskini ndani ya nchi na kuifanya AI ipatikane kwa watu wote.

Deep Aman Gill, kiongozi wa kiteknolojia wa India aliyevaa turban ya bluu na suti, anaongea katika mkutano wa AI Summit USG, akiashiria kwa mikono yake.

Deep Aman Gill akizungumza katika mkutano wa AI Summit USG

“Mkusanyiko wa nguvu za kiuchumi na kiteknolojia ndilo jambo linalotusumbua zaidi katika Umoja wa Mataifa,” amesema Bwana. Gill. “Tumeona hali kama hii wakati wa mapinduzi ya viwanda yaliyopita, ambapo waliokosa kutumia nishati ya mvuke walijikuta nyuma kwa miaka 50 kimaendeleo. Hatuwezi kuruhusu hilo litokee tena.”

Licha ya tahadhari hizo, ameeleza kuwa baadhi ya maeneo tayari yana mikakati ya kunufaika na AI na kuepuka kubaki nyuma. “Ninaona hili katika Asia ya Kusini Mashariki, sehemu nyingi za Afrika na nchini India, ambapo serikali inaongoza kwa kutoa ruzuku ya upatikanaji wa AI kwa watafiti, wabunifu na kampuni ndogo.”

Ingawa Mkutano wa Athari za AI ai AI Impact si tukio rasmi la Umoja wa Mataifa, Bwana. Gill ameshiriki katika kuandaa ajenda yake na anaona kuwa ni hatua muhimu kuelekea usimamizi wa kimataifa. “Inatia moyo kuona msisitizo wa kuziba pengo la AI, kujenga uwezo na kuwashirikisha wananchi kwa mtazamo wa kidemokrasia kuhusu teknolojia hii.”

Nini cha kutarajia katika mkutano

• Wiki ya AI Impact inafanyika kuanzia 16 hadi 20 Februari katika Kituo cha Mikutano cha Bharat Mandapam mjini New Delhi
• Itawaleta pamoja viongozi wa dunia, watunga sera, makampuni ya teknolojia, wabunifu na wataalamu kujadili uwezo wa mageuzi wa AI katika utawala, ubunifu na maendeleo endelevu
• Katibu Mkuu António Guterres atahutubia mkutano huo Alhamisi tarehe 19 Februari
• Mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa yataandaa matukio ya kando kuonesha matumizi ya AI kwa manufaa ya kijamii

Mashirika hayo ni pamoja na:
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), UN Women,Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF, Shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani (WHO),Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi  (UNFPA), Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Teknolojia za Kidijitali na Zinazochipukia.

Picha ya karibu ya chip inayoangaza ya AI kwenye bodi ya mzunguko wa kompyuta na taa ya kijani.

© Unsplash/Immo Wegmann

Mifumo ya AI itasaidia katika uchambuzi wa takwimu, kufanya maamuzi, automatisering, na optimization.

Umoja wa Mataifa na AI

Hizi ni baadhi ya kazi zinazofanywa katika mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa ili kupunguza ukosefu wa usawa wa kimataifa kwa kushughulikia mgawanyo usio sawa wa manufaa ya AI na kuimarisha uwezo wa kidijitali katika nchi zinazoendelea:

• Mkataba wa Kidijitali wa Kimataifa, mfumo wa kimataifa wa ushirikiano wa kidijitali na usimamizi wa AI, uliopitishwa na viongozi wa dunia katika Mkutano wa Zama Zijazo wa 2024
• Kanuni za Matumizi ya Kimaadili ya AI katika Mfumo wa Umoja wa Mataifa
• Jopo la Ushauri la Ngazi ya Juu kuhusu AI na Majadiliano ya Kimataifa kuhusu Usimamizi wa AI
• AI for Good, jukwaa kubwa zaidi la Umoja wa Mataifa linalolenga kupanua suluhisho za vitendo vya AI ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu
• Pendekezo la UNESCO kuhusu Maadili ya AI (2021), mfumo wa kwanza wa kimataifa wa maadili ya AI uliopitishwa na Nchi Wanachama 193
• Generation AI ya UNICEF, juhudi ya kimataifa ya kujenga ushahidi, kuunda sera na kuendeleza suluhisho za AI zinazolinda haki za mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *