Katika sekta ambayo ukuaji wa kasi wakati mwingine huweza kuja kwa gharama ya nidhamu ya kiutendaji, MUA Insur­ance (Tanzania) Limited inaamini kwamba uku­aji lazima uwe endelevu, uzingatie kanuni na ubora.

Hivi karibuni kampuni hiyo iliandaa tukio lake la tuzo za mawakala wa bima lililofanyika Feb­ruari 13, 2026. Tukio hilo liliwakutanisha mawakala bora wa bima kutoka mae­neo mbalimbali ya nchi pamoja na viongozi wa juu wa kampuni, kwa lengo la kusherehekea mafanikio na kuimarisha mwelekeo wake wa kimkakati.

Zaidi ya kuwa hafla ya kawaida ya utoaji tuzo, tukio hilo lilidhihirisha dhamira ya kampuni hiyo katika kuzingatia misingi imara ya utawala bora, viwango vya kitaaluma na upanuzi wenye uwajibikaji ndani ya soko la bima la Tanzania linalozidi kuwa na ushindani.

Ikiwa na mtandao wa zaidi ya mawakala 100 wanaofanya kazi nchi nzima, wakisaidiwa na matawi 10, vituo vinne vya mauzo pamoja na ofisi kuu iliyopo Dar es Salaam, MUA Tanzania inaendelea kupanua wigo wake kitaifa huku ikiendelea kuzinga­tia kwa makini kanuni za tathmini ya hatari (under­writing) na masharti ya udhibiti wa sekta.

Mtandao wa mawakala wa bima unaendelea kuwa nguzo muhimu katika mka­kati wa kampuni hiyo husu­sani katika utoaji wa bima ndogo, ukiwa kiungo kikuu kati ya kampuni na wateja wake wanaoongezeka siku hadi siku.

Katika hafla hiyo, tuzo zilitolewa kwa mawakala wa bima walioonyesha utendaji bora kwa kuzinga­tia vigezo mbalimbali, si tu kiwango cha uzalishaji wa michango ya bima (pre­mium), bali pia ubora wa bima kwa wateja, uwezo wa kuwabakiza wateja, weledi na ufuataji wa kanuni za udhibiti. Utaratibu huo wa utoaji tuzo unaakisi falsafa pana ya kampuni kuwa, mafanikio hupimwa kwa uendelevu, si kwa wingi wa mauzo pekee.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mtendaji Mkuu wa MUA Insurance (Tanza­nia) Limited, Jérôme Katz, amesisitiza umuhimu wa kimkakati wa mtandao wa mawakala katika kukuza ukuaji wa kampuni hiyo.

“Mawakala si njia ya usambazaji tu. Wao ni uti wa mgongo wa mfumo wetu wa biashara. Ukua­ji endelevu hauhusu tu kuongeza uzalishaji, bali ni kujenga bima zenye ubora, kuheshimu miongozo ya tathmini ya hatari na kuz­ingatia kikamilifu kanuni zote za udhibiti. Utendaji na nidhamu lazima viende sambamba.” amesema Katz.

Jioni hiyo pia ilitumika kama kumbukumbu ya safari ya kampuni hiyo katika soko la Tanzania. Ikiwa ni sehemu ya MUA Group, inayotambuliwa kwa uimara wa kifedha na uthabiti kwa muda mrefu, kampuni hiyo liliingia Tan­zania mwaka 2014 kama mbia mkuu wa kampuni ili­yokuwa ikifanya kazi chini ya chapa ya Phoenix.

Ikiwa inajulikana kama Phoenix of Tanzania hadi mwaka 2023, kampuni hiyo ilikamilisha mchakato wa kubadili jina na chapa kuwa MUA Insurance (Tan­zania) Limited, ikiwa ni sehemu ya mkakati mpana wa kuoanisha chapa katika ukanda wa Afrika Mashari­ki.

Sambamba na mkakati wake wa kuendelea kupa­nuka, chapa ya MUA nchini Tanzania hivi karibuni imeimarisha uwepo wake sokoni kupitia kuanzishwa kwa MUA Life Tanzania, kampuni tanzu inayojikita katika bima za maisha, hatua inayopanua wigo wa bidhaa za kampuni hiyo na kuimarisha dhamira yake ya muda mrefu nchini.

Katika kuhitimisha haf­la ya utoaji wa tuzo hizo, ilisisitizwa kuwa, MUA Tanzania imejengwa kupi­tia ushirikiano, nidhamu, uzingatiaji wa kanuni na mtandao imara wa mawakala nchini kote.

Katika soko linalozidi kutawaliwa na ushindani, kampuni hiyo inajipam­banua si tu kama kampuni inayokua, bali kama taasisi yenye mifumo thabiti na mtazamo wa mbele inay­olenga kufikia malengo makubwa ya kibiashara na umakini wa kitaalamu pamoja na utendaji ende­levu.

Kupitia misingi imara ya utawala bora, umakini wa kitaalamu na uwekezaji endelevu, MUA Tanzania inaendelea kujiimarisha kama mtoa huduma wa bima anayeaminika na mwenye maono ya muda mrefu katika soko la Tan­zania.

Washindi wa tuzo za mawakala wa bima mwaka huu ni pamoja na: 1.Fixers Insurance Agency

2. Manyeki Insurance Agency

3. Scan Insurance and Gen Services Ltd

4. JJS Insurance Agency

5. Triple C Insurance Agency

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *