Chanzo cha picha, Getty Images
Muda wa kusoma: Dakika 1
Beki wa Nottingham Forest Murillo anajiandaa kukihama klabu hicho msimu huu wa joto huku Chelsea na Liverpool zikionyesha nia ya kitaka kumsajili Mbrazil huyo wa miaka 23. (Teamtalk)
Klabu ya Napoli imeanza mazungumzo na wawakilishi wa kiongo wa Scotland Scott McTominay, 29, kuhusu mpango wa kurefusha mkataba wake Italia hadi 2030. (Corriere dello Sport – kwa Kiitaliano)
Manchester City italazimika kulipa kati ya pauni mlioni 60-70 kumsajili kiungo wa kati wa England na Nottingham Forest Morgan Gibbs-White, 26, msimu wa joto. (Football Insider)
Chelsea na Tottenham wana nia ya kumsajili beki wa kati wa Bayern Munich kutoka Korea Kusini Kim Min-jae, 29. (CFBayernInsider)
Winga wa RB Leipzig wa Ivory Coast Yan Diomande, 19, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kwenda Liverpool, anasema klabu hiyo ya Anfield ndiyo klabu babake anaihusudu. (Bild via Goal)
Lakini meneja wa Bayern Munich Vincent Kompany anataka viongozi hao wa Bundesliga kuwashinda wapinzani wao waLigi ya Englandili kumsajili Diomande katika msimu wa joto. (Fabrizio Romano)