
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili siku ya Jumatatu jioni, Februari 16, nchini India kwa ziara rasmi ya siku tatu inayolenga kuimarisha ushirikiano wa karibu ambao tayari upo, huku kukiwa na matarajio ya mkataba mkubwa wa ndege 114 za kivita za Rafale. Mkutano wa kilele kuhusu Akili Bandia, unaoongozwa kwa ushirikiano na nchi hizo mbili, pia uko kwenye ajenda.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu maalum huko New Delhi, Aabla Jounaïdi
“Tunakwenda India! Siku tatu kutoka Mumbai hadi New Delhi ili kuimarisha zaidi ushirikiano wetu wa kimkakati. Viongozi wetu wa biashara na wadau wa kiuchumi, viwanda, kitamaduni, na kidijitali wanaoleta uhusiano kati ya nchi zetu katika njia inayoonekana sana. Pamoja, tutaendeleza ushirikiano wetu zaidi. Tutaonana kesho, rafiki yangu mpendwa Narendra Modi!” rais wa Ufaransa aliandika kwenye mtandoa wa kijamii wa X.
India na Ufaransa zimeazimia kuonyesha uhusiano ulioimarishwa, kuanzia na sekta ya ulinzi, kipaumbele cha kitaifa nchini India.
Wiki iliyopita, New Delhi ilitangaza nia yake ya kununua ndege mpya za kivita za Rafale, labda 114, pamoja na zile 62 zilizoagizwa tayari. Huu ungekuwa mkataba wa kihistoria, lakini majadiliano ya kiufundi yanaendelea, Ikulu ya Élysée imesema.
Ujumbe mkubwa wa kiuchumi unaambatana na rais wa Ufaransa. Lengo lao ni ulinzi, utafiti, usafiri, nishati, Akili andia, na filamu.
India ni mshirika wa tatu kwa ukubwa wa biashara wa Ufaransa barani Asia, lakini hii inaweza kuwa muhimu zaidi tangu makubaliano ya biashara huria yaliposainiwa mwezi uliopita na Umoja wa Ulaya (EU).
Kufufua uhusiano wa kimataifa unaopingwa na Washington
Mbali na mikataba mikubwa inayowezekana, Ikulu ya Élysée inataka kupeleka uhusiano wake na India, mshirika wa kimkakati, katika ngazi inayofuata. Kwa kukabiliana na Marekani na China, lengo ni kuonyesha kwamba njia nyingine ipo.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akiwa ni raisa wa G7, na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, akiwa mwenyekiti wa BRICS mwaka huu, wanajitahidi kwa pamoja kufufua mfumo wa pande nyingi, ambao umepingwa, hasa na Washington.
Kwa mfano, siku ya Alhamisi, Narendra Modi na Emmanuel Macron watazindua mkutano wa Akili Bandia huko New Delhi, ulio wazi kwa nchi za Kusini mwa Dunia na kuwasilishwa kama unaohudumia manufaa ya wote. Kituo cha afya cha Ufaransa na India pia kitazinduliwa katika tukio hilo.