#HABARI: Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Moses Kusilukwa amesema matumizi ya TEHAMA ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali kutokana na kurahisisha huduma kwa Wananchi.
Amesema hayo wakati akiongea kwenye Kikao kazi cha sita cha Serikali Mtandao (e-Gov), Jijini Arusha.
Amebainisha kuwa TEHAMA imekuwa ni nguzo ya mabadiliko ya kiutendaji yenye kuongeza ufanisi wa huduma na maendeleo kwa watu nchini.
Aidha, amefurahishwa na kupongeza jitihada za Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kutokana na matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU).
Pongezi hizo zimetolewa wakati Mrajis wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akitoa maelezo ya MUVU katika Banda la Maonesho la Tume katika kikao kazi hicho.
Tume ni miongoni mwa Taasisi zilizotambuliwa kwa matumizi ya TEHAMA katika uendeshaji wa shughuli za Ushirika na udhamini wa Kikao hicho.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania