#HABARI: Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Jumanne Februari 17.2026 imesikiliza mapingamizi yaliyowekwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohamed na wenzake wawili dhidi ya Katibu Mkuu na Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA katika kesi ya usawa kwenye mgawanyo wa mali kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Katika mapingamizi hayo, waleta maombi wanapinga maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu ambaye anaomba kujumuishwa kama sehemu ya wajibu maombi wa kesi hiyo,

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, na Kiongozi wa jopo la Mawakili wa CHADEMA kwenye kesi hiyo Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala amewaeleza Waandishi wa Habari kuhusiana na kilichotokea Mahakamani leo kwenye usikilizwaji wa mapingamizi hayo.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Jaji anatarajiwa kutoa maamuzi ya mapingamizi hayo Machi 03, 2026.

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *