#HABARI: Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), ikishirikiana na Jeshi la Polisi, imefanikiwa kukamata kilogramu 299.8 za mirungi na kuteketeza ekari 203 za mashamba ya zao hilo katika Wilaya ya Same, Kilimanjaro.
Operesheni hiyo maalum iliyofanyika kati ya Februari 10 na 16, 2026 katika vijiji vya Marieni na Mhero, imesababisha pia kukamatwa kwa watuhumiwa saba wanaohusika na uhalifu huo wa dawa za kulevya.
Pamoja na jitihada za Serikali za muda mrefu za kutoa elimu na kuleta miradi ya maendeleo, bado kuna watu wachache wanaoendelea kukaidi sheria kwa kujihusisha na kilimo na biashara ya mirungi.
Mamlaka imesisitiza kuwa haitavumilia vitendo hivyo na itaendelea kushirikiana na viongozi wa ngazi zote, kuanzia vijijini hadi mkoani, ili kuhakikisha operesheni endelevu zinafanyika na tatizo la mirungi linadhibitiwa kikamilifu mkoani Kilimanjaro.
Mwisho, wananchi wanaombwa kuendelea kutoa ushirikiano katika mapambano haya dhidi ya dawa za kulevya kwa manufaa ya maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
DCEA imeweka wazi kuwa ushiriki wa kila mdau ni muhimu katika kutokomeza biashara hii haramu na kulinda nguvu kazi ya nchi, huku ikiahidi kuendelea kutoa elimu na kusimamia sheria bila kulegalega kote nchini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.