#HABARI: Mamlaka za kidini nchini Saudi Arabia, imetangaza kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani baada ya kuonekana kwa mwezi mwandamo nchini humo hii leo.

Kwa mujibu wa mamlaka nchini humo ni zimesema Ramadhani itaanza Februari 18 kufuatia kuonekana kwa mwezi Februari 17, ambayo ilikuwa siku ya 29 ya Shaaban katika kalenda ya Kiislamu.

Kwa mara ya kwanza, Teknolojia ya kisasa ilitumika katika Kituo cha Uangalizi wa Anga cha Sudair kusaidia katika zoezi la kuutazama mwezi mwandamo, ambapo Mtaalam wa kuandama mwezi, Abdullah Al-Khudairi, amethibitisha, hivyo kwa tangazo hilo linaashiria mwanzo wa mwezi mtukufu ambao Waislamu duniani kote hushiriki katika kufunga, kusali na kufanya ibada mbalimbali.

Katika kurahisisha mchakato, Saudi hivi karibuni ilizindua Kituo cha Uchunguzi wa Tamir, kulingana na Shirika la Habari la Saudi (Saudi Press Agency), kituo hicho kimepewa jukumu la uchunguzi rasmi wa mwezi na ufuatiliaji wa kilele cha mwezi, likilenga hasa uchunguzi unaohusiana na Ramadan na kufuata viwango vilivyowekwa vya Kisayansi.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *